UMAKI

UMAKI SOCIAL DAY
Umoja wa Wakina Mama (UMAKI) wa Mt. Batholomayo Ubungo umeandaa matembezi ya UTALII wa ndani itakayofanyika ktk Mbuga za WANYAMA SAADAN BAGAMOYO kuanzia tar. 18-19.
Zaidi ya Utalii wa Ndani wakinamama watabadirishana mawazo ktk mapumziko hayo kwa kuandaa mikakati mipya ya kifamilia, kijamii, kiroho, na kufanya Uinjilisti wa Kumtangaza Kristo.

**Uongozi wa UMAKI
MT. BATHOLOMAYO UBUNGO**

UMAKI ni chama cha Wanawake katika kanisa la Anglikana hapa Tanzania. Hiki ni kifupisho cha maneno UMOJA WA MAMA WA KIKIRISTO, kwa lugha ya Kiingereza chama hiki huitwa MOTHER UNION kwa kifupi ni MU. Chama/Taasisi hii ni muhimu, imeenea na inatambuliwa na makanisa yote ya Kianglikana ulimwengu kote

Chama hiki kilianzishwa na mke wa Padre/Kasisi/Mchungaji aliyeitwa Mama Mary Sumner, mwaka 1886 kule Uingereza, baada ya kuona uzito wa kazi za mumewe hasa kuhusu huduma ya wanawake ndani ya Kanisa. Kwa sababu hiyo,mama huyu na wenzake aliowashawishi walijadili njia mbalimbali za kuboresha huduma kwa wanawake katika Kanisa na jamii kwa ujumla.

Chama hiki ni kwa ajili ya wanawake wa wakikristo hususani Waanglikana wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. Mama muumuni wa madhehebu mengine anaweza kujiunga katika chama hiki kwa kukubali makusudi ya chama hiki na zaidi sana kwa kibali maalumu kutoka kwa Askofu wa Dayosisi alipo.

Inakadiriwa kuwa na wanachama 80 – 100 hapa tawini. Si rahisi kupata takwimu sahihi wanachama kwa sababu: Wengi hawatoi Ada ya Mwaka, na wengi hawahudhurii darasa la Akina mama siku za Jumanne.